Buha FM Radio
Buha FM Radio
November 25, 2025, 11:18 pm

NGOs katika Wilaya ya Kasulu wapongeza jitihada za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kuwapa elimu na kuwakumbusha kanuni na sheria za kodi kupitia semina iliyoendeshwa katika wilaya hiyo.
Na; Sharifat Shinji
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Kigoma imezikumbusha taasisi binafsi (NGOs) kufuata mashariti waliyopewa kipindi wanaomba kusajiliwa kwa taasisi zao ili kuendelea kutoa huduma katika jamii kwa mijibu wa kanuni na sheria zilizowekwa.
Akizungumza na Buha FM Radio baada ya semina iliyofanyika Leo kwenye ukumbi wa Serengeti katika Halmashauri ya Mji Kasulu Meneja Msaidizi mkoa- Ukaguzi na ufuatiliaji wa TRA Ndg. Fredrick Tweve amesema wanaendelea kutoa elimu ya kikodi kwa taasisi hizo huku maoni na changamoto zilizowasilishwa wakizichukuwa kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha mratibu wa Semina hiyo Bi. Makilo Lukurunge amesema elimu waliyoitowa kwa taasisi hizo itasaidia kuongeza mapato kwa serikali na kuwashauri wadau wanaotaka kuanzisha NGOs kupita sehemu sahihi kwa ajili ya elimu na kupata unafuu wa kodi kwenye swala la uendeshaji wa taasisi.
Nao baadhi ya wadau wa mashirika mbalimbali akiwemo Jovita Joakimu kutoka shirika la kilimo la Kickstart International na Robison Lusanzu kutoka shirika la mazingira la EarthCare Foundation wameeleza namna semina hiyo ilivyowapa mwanga wa namna ya kutambua haki na kuzingatia sheria za kulipaji kodi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeahidi kuendelea kuwapa elimu wadau na viongozi mbalimbali wa taasisi mbalimbali sisizo za kiserikali (NGOs) kwa kuwakaribisha ofisini pamoja na kuendesha semina kupitia vyombo vya habari.