Buha FM Radio
Buha FM Radio
October 1, 2025, 4:36 pm

Kuelekea msimu wa mvua baadhi ya wafanyabiashara na wakazi katika mtaa wa soko la Kwashayo katika Halmashauri ya Mji Kasulu wameomba kutafutiwa suluhisho la kudumu kuhusu Dampo la taka linalopatikana maeneo hayo.
Na:Irene Charles
Baadhi ya wafanyabiashara na wakazi katika soko la Kwashayo katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wamesema uwepo wa dampo la taka katika eneo hilo imekuwa changamoto kwao kutokana na kujaa kwa uchafu na kusababisha halfu kali katika maeneo hayo.
Wakizungumza na Buha FM radio wamesema wakati huu wa kiangazi upepo unapelekea uchafu kufika katika biashara zao huku uchomaji wa taka hizo husababisha moshi ambao sio salama kwa afya hasa kwa wakazi wa maeneo hayo ya karibu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa eneo hilo Jackson Emily Magambo amesema toka mwezi Mei waliahidiwa kutolewa kwa dampo hilo huku akishauri taka hizo ziondolewe na magari ya taka kuliko kuchoma taka katika mazingira hayo ya biashara na makazi ya watu.
Aidha Ndg. Jackson ameuomba uongozi husika pamoja na wizara ya afya kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo ilikuepukana na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na watoto kucheza kwa wingi katika mazingira hayo.
Licha ya buha fm radio kulipoti kila mara kuhusu hali ya uchafuzi wa mazingira na utupaji wa taka Hovyo karibu na makazi bado imekuwa nichangamoto kukabiliana na hali hiyo April 30, 2025 Buha fm Radio ilichapisha habari kuhusu utupaji taka katika maeneo ya makazi ya watu lakini bado ni nimfupa mgumu kutatuliwa changamoto katika makazi ya watu.
