Buha FM Radio

Kasulu DC yapata mwarobaini wa uhalifu

September 20, 2025, 2:46 am

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2025 akieleza kuhusu huduma za kipolis zilivyo na umhimu katika jamii. Picha na Sharifat Shinji.

Halmashauri imezindua kituo cha polis Nyakitonto kitakachowezesha kusaidi wananchi wa Halmashauri hiyo kutatua changamoto zao za kipolis na kiusalama kwa karibu tofauti na zamani ambapo walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Na; Sharifat Shinji

Kiongozi mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ndg.Ismail Ussi amezindua kituo cha Polis Nyakitonto katika Halmashauri ya Kasulu mkoani Kigoma na kusema kituo hicho kitumike kwa kuwasaidia Wananchi wa Halmashauri hiyo.

Kituo hicho kimezinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru huku kiongozi huyo ameeleza namna ambavyo huduma ya polisi ilivyo mhimu katika jamii na kuwasisitia wananchi kutoa ushirikiano wao na Jeshi la polis pamoja na kulinda usalama, amani na utulivu katika maeneo yao.

Sauti ya Ndg.Ismail Ussi kiongozi wa mbio za Mwenge 2025.
Sauti ya Ndg.Ismail Ussi kiongozi wa mbio za Mwenge 2025 akieleza kuhusu huduma za kipolis zilivyo na umhimu katika jamii. Picha na Sharifat Shinji.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Isack Mwakisu amesema sababu ya kujenga kituo cha polis eneo la Nyakatondo ni kuhakikisha maswala ya usalama yanasogezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ili jamii ipate huduma ya kiusalama kwa masaa 24 tofauti na zamani ambapo walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Isack Mwakisu.

Katika nyingine Mhandisi Raulent msakila wakati akisoma taarifa ya mradi amesema kukamilika kwa mradi huo utaenda ktatua changamoto mbalimbali ikiwemo kumaliza tatizo la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Sauti ya Mhandisi Raulent msakila wakati akisoma taarifa ya mradi.

Mradi huo umegharimu zaidi ya Milioni 100 kupitia mapato ya Ndani ya Halmashauri ukiwa umechukuwa zaidi ya miaka miwili kukamilika. Mbio za mwenge wa uhuru 2025 zimeambatanana na Kauli mbiu isemayo “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na utulivu”

Mwenge wa Uhuru 2025 katika Wilaya ya Kasulu katika utekelezaji wa uzinduzi wa Miradi Mbalimbali wilauani humo. Picha na Sharifat Shinji.