Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 19, 2025, 6:53 pm

Ujenzi wa Wodi ya wazazi katika Kituo cha afya Mwami Ntale katika Kata ya Heru Juu umekamilika kwa asilimia 90% ambapo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Na; Sharifat Shinji.
Wakazi wa kata ya Heru Juu katika Halmashauri ya mji Kasulu wamefurahishwa baada ya uzinduzi wa jengo la Wodi ya wazazi na jengo la Kufulia katika kituo cha afya Mwami Ntale huku wakitaja changamoto walizokuwa wanazipiti kablaya huduma hiyo haijasogezwa karibu na makazi yao.
Hayo yamejili wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndg. Ismail Ussi akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la Wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Mwami Ntale kata ya Heru Juu katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma siku ya tarehe 18, mwaka huu.

Aidha kiongozi wa Mbio za Mwenge baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa jengo hilo katika kituo cha afya Mwami Ntale, mradi unaotekelezwa na fedha za Serikali amesisitiza majengo hayo yanakamilika kwa wakati na kuanza kutumika kwa Kuwasaidia wananchi katika huduma za kiafya.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo la Wodi ya wazazi na Jengo la kufulia katika kituo cha afya Mwami Ntale Mganga Mfawidhi Mgoba John amesema ujezi wa jengo la Wodi ya wazazi limekamilika kwa asilimia 90% huku Jengo la kufulia likiwa limakamilika kwa ailimia 95% huku akitaja mradi huo utakamilika Septemba 30 mwaka huu.
Halmashauri ya Mji Kasulu ina jumla ya Kata 15, ambapo ilikuwa na jumla ya vituo vya afaya viwili ambavyo ni Kabanga na Nyasha kituo cha Afya hivyo kukamilika kwa kituo cha afya Mwami Ntale kilichogharimu milioni 300 kutoka serikali kuu itafanya kufikisha idadi ya vituo vitatu katika Halmashauri ya Mji Kasulu.
