Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 19, 2025, 5:33 pm

“Kiukweli uwepo wa soko la Kwashayo inatufanya sisi tushindwe kupata wateja serikali ikamilishe soko hili wafanya biashara waliopo kule wahamie hapa maana wakiwepo kule sisi hatuuzi kabisa hali hii inapelekea kushindwa hata kuendesha familia zetu” Alisikika mmoja ya wafanya biashara akizungumza.
Na; Irene Charles
Baadhi ya Wafanya biashara wa mazao katika soko Mazao Mnadani lililopo Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wamesema hali ya ngumu ya mauzo mahindi imekuwa ni changamoto kwao kutokana na uwepo wa soko la Kwashayo hali inayopelekea uchaje wa wateja katika soko hilo.
Wamebainisha hayo walipotembelewa na Buha FM radio Kutaka kufahamu hali ya mauzo katika soko hilo na kuiomba serikali kukamilisha ujenzi wa soko ili iwasaidie kuongeza na kurahisisha upatikaji wa wateja wa kutosha katika maeneo yao ya biashara.
Eshodi Rajabu ni mfanyabiashara wa nafaka za mahindi na maharage amesema upatikanaji wa mahindi kwa sasa ni mzuri lakini changamotoo ni masoko kwani hawana wateja wa kudumu katika soko hilo.

Aidha katibu wa wafanyabiashara katika soko la mazao Mnadani ndug.Nelson Msyomole amesema serikali kupitia mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wamesema mpaka kufika mwezi wa 12 ujenzi wa soko jipya utakuwa umekamalika.
Katika hatua nyingine Bw.Nelson amesema baada ya soko la Mnadani kukamilika wafanyabiashara wa soko la Kwashayo watahamia katika soko jipya kwa sababu litakua linatabulika kisheria,huku akiwaasa kufanya usafi kila siku katika maeneo yao ya biashara.
Kwa muujibu wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Desemba 11, 2024 kilijadili kuhusu usitishwaji wa soko la Kwashayo kufanya shughuri za biashara majira ya asubuhi na kulipa uhalali soko hilo majira ya saa 12 jioni baada ya soko la Mazao Mnadani kufungwa lakini hadi sasa masoko yote mawili yanafanya kazi kwa masaa sawa hali inayopelekea soko la Mnadani kuwa na Mdororo wa wateja hali inayopelekea wafanya biashara kushindwa kuendesha shughuli za biashara katika soko hilo.
