Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 18, 2025, 10:18 pm

“Serikali kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwajali wadau wa elimu na idara ya elimu kwa ujumla katika kutekeleza miradi itakayosaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuwatengenezea walimu mazingira mazuri ya kufundishia” Amesema Ndg. Ussi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Ismail Ussi amezindua nyumba ya walimu two in one 2_1 katika shule ya sekondari Msambala katika Halmashauri ya Mji Kasulu nyumba itakayowasaidia watumishi kufundisha wakiwa katika makazi bora ya kuishi.
Uzinduzi huo umefanyika Leo Septemba 18 katika Eneo la Shule hiyo ikiwa ni mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma huku kiongozi wa mbio za mwenge akiwasisitiza walimu kutunza miundombinu yote inazotekelezwa na serikali mkuu.
Aidha Ussi amekipongeza kitengo cha kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwa kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari, msingi na vikundi mbalimbali ikiwemo wajasiliamali na Maafisa usafirishaji maalufu Bodaboda kwa kuunda vikundi vya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU ili kutokomeza tatizo la rushwa nchini.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo Mkuu wa shule ya sekondari Msambala Mwl. Werema Mashenene kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Mji amesema mradi huo umegharimu Million 110 hadi kukamilika.

Sanjari na uzinduzi na kuweka Jiwe la msingi la nyumba ya walimu katika Shule hiyo, pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amezindua na kuweka jiwe la msingi la klabu ya wanafunzi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU katika shule hiyo yenye wanachama zaidi ya 100 katika shule hiyo.
