Buha FM Radio
Buha FM Radio
September 18, 2025, 12:17 am

“Nina imani kubwa kuwa jengo hili litawasaidia wananchi na watoa huduma mtatoa huduma bora na nzuri kwa wananchi wote wa Halmashauri hii pia litaongeza chachu ya maendeleo katika maeneo haya” Amesema Ussi.
Na; Sharifat Shinji
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imezindua jengo la Baba, mama na mtoto katika Hospital ya
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu iliyopo katika eneo la Nyamnyusi, ambapo jengo hilo litasaidia wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu katika huduma za kiafya kwa Baba, Mama na Mtoto tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wanalazimika kuchanganywa na wagonjwa wengine wakawaida.
Uzinduzi wa Jengo la Huduma ya baba, mama na mtoto limezinduliwa Septemba 17 na kiongozi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Ismaili Ussi na kusema jengo hilo litumike kwa kutoa huduma
bora kwa wananchi huku akisisitiza watoa huduma za afya kutoa huduma kulingana na weledi wao.
Nao baadhi ya wananchi kutoka Halmashauri hiyo wameshukuru jengo hilo kuzinduliwa huku wakisema huduma sasa zitatolewa wakiwa kwenye jengo lao tofauti na zamani ambapo walikuwa wakilazimika kuchangamana na wagonjwa wengine.

Sanjari na hayo Mwenge umezindua Barabara ya Lami yenye urefu wa nusu Kilomita 0.5 kutoka barabara
kuu hadi Hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu huku wananchi wakisisitizwa kulinda rasilimali za
zote zinazotekelezwa na Serikali.

Awali mkuu wa Wilaya Kasulu mhe. Kanal Isack Mwakisu amesema mbele ya Kiongozi wa mbio za
mwenge wa Uhuru kuwa ujenzi wa jengo hilo umetumia zaidi ya milioni 500 ambao umesimamiwa
kikamilifu na Mamlaka ya Barabara Vijijini TARURA.
Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu umezindua miradi 7 iliyogharimu
shilingi Bilioni 1.47 ambapo miradi yote hiyo imepitiwa na mwenge wa uhuru kwa ukaguzi,uzinduzi na
kuwekewa jiwe la msingi Septemba 17 mwaka huu.
