Buha FM Radio

Wafanyabiashara walia ujenzi wa soko Mnadani

August 9, 2025, 11:44 am

Baadhi ya Mazao ya Nafaka soko la Mnadani Halmasahuri ya Mji Kasulu. Picha na Paulina Majaliwa.

Wamezitaja changamoto zingine kuwa ni vumbi pamoja na jua kali wanalokumbana nalo kutoka na soko la Mnadani kutokamilika ujenzi wake hali inayowalazimu kufanyia kazi hiyo nje ya majengo.

Na Emily Adam

Wafanyabiashara wa mahindi na maharage rejareja katika soko la mnadani Halmashauri ya Mji  Kasulu mkoani Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa mauzo pamoja na ukosefu wa wateja hali inayowapelekea kukosa kipato cha kuhudumia familia zao.

Wamebainisha hayo wakati wakiongea na Buha FM Radio sokoni hapo juu ya changamoto wanazokumbana nazo wakati wakiendesha shughuli hiyo ya biashara za mazao ya nafaka katika eneo hilo.

Miongoni mwa wafanyabiashara hao  Editha Damiano na Beatrice Medani wamezitaja changamoto zingine kuwa ni vumbi pamoja na jua kali wanalokumbana nalo kutoka na soko la manadani kutokamilika ujenzi wake hali inayowalazimu kufanyia kazi hiyo nje ya majengo.

Sauti za Wafanyabiashara

Aidha wameiomba serikali wilayani Kasulu kuharakisha na kukamilisha ujenzi wa soko hilo ili wafanyabishara wa mazao ya kilimo wafanye kazi hiyo kwa ufanisi zaidi hali itayosaidia upatikanaji wa wateja na kuongeza kasi ya mzunguko wa biashara zao na kujipatia kipato kitakachowawezesha kuhudumia familia zao.

Kutokana na soko la kuuzia mazao ya chakula la mnadani kutokakamilika wafanyabiashara na watumiaji wa soko hilo wamekuwa wakilazimika kulitumia katika mazingira magumu ya kuchomwa na jua pamoja na kukumbana na vumbi ambayo wakati mwingine huigia kwenye bidhaa hali inayopelekea kukosekana kwa wateja wa bidhaa wanazouza.