Buha FM Radio
Buha FM Radio
July 31, 2025, 2:31 pm

Dkt. Kudra ameshauri kila mtu anatakiwa kuwa na utaratibu ya kwenda kituo cha afya kuangalia afya yake pia amesema ukiona dalili hizo unatakiwa kufika kwa wataalamu kwaijili ya kupatiwa tiba ya kisalojia na kupatiwa dawa.
Na Irene Charles
Changamoto za kimahusiano, Familia, na hali ngumu ya maisha zinatajwa kuwa miongoni mwa sababu kubwa za kuongezeka kwa matukio ya kujinyonga sehemu mbalimbali nchini.
Hayo yameelezwa leo na wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wakati wakizungumza na buha FM radio na kusema kuwa wivu wa kimapenzi umekuwa ukiwatesa sana wanandoa waliowengi hasa wanaume na wengine wakijikatia tamaa kutokana na matatizo yanayowasibu.
Kwa upande wake mtaalamu wa afya ya akili (saikolojia) Dkt. Kudra Hisa Karebela kutoka hospitali ya Mlimani Halmashauri Mji Kasulu amesema mtu anapofikia maamuzi ya kujiua au kufikiria kufanya kitendo hicho hiyo ni dalili ya ugonjwa wa afya ya akili.
Dkt. Kudra amesema magonjwa mtu anayoweza kupata kutokana na afya ya akili ni sonona, hofu iliyopitiliza, kukosa usingizi wa kutosha, kuona na kusikia vitu ambavyo wengine awavioni kwa watoto kukosa utulivu kujikojolea.
Aidha Dkt Kudra amesema ugonjwa wa sonona kwa asilimia kubwa unawapata wanawake ambapo dalili zake ni kujitenga, kulia sana na kuwa na hasira, kupoteza kumbukumbu, hofu iliyopitiliza, kukosa usingizi na kusababisha kukosa hamu ya kula na wengine kula kupitiliza.
Dkt. Kudra ameshauri kila mtu anatakiwa kuwa na utaratibu ya kwenda kituo cha afya kuangalia afya yake pia amesema ukiona dalili hizo unatakiwa kufika kwa wataalamu kwaijili ya kupatiwa tiba ya kisaikolojia na kupatiwa dawa.