Buha FM Radio
Buha FM Radio
July 8, 2025, 6:11 pm

Ili kuepukana na ugonjwa wa bawasiri suluhisho kwa kunywa maji ya kutosha angalau kila siku glasi sita au nane kwa siku, kula mbogamboga na matunda, kuepuka kukaa au kusimama sehemu moja kwa muda mrefu na kufanya mazoezi.
Na Irene Charles
Bawasiri sio laana wala sio aibu bali ni ugonjwa unao sababishwa na sababu mbalimbali kama kukaa na kusimama kwa muda mrefu, uzito uliopitiliza, kula kwa wingi nyama nyekundu na vidonda vya tumbo, ngiri na chango.
Hayo yamesema na mtaalamu wa afya ya uzazi Dkt. Suzana Geazi Ngogo kutoka Hemocare Clinic wakati akizungumza na Buha FM Radio ambapo amesema dalili za bawasiri ni kupata muwasho mkali, kujitokeza kinyama sehemu ya aja kubwa pamoja na kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia.
Kwa upande wao Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wamesema kuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huo huku wakiwaomba wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu ya kutosha.
Ili kuepukana na ugonjwa wa bawasiri Dkt. Suzan amesema suluhisho kwa kunywa maji ya kutosha angalau kila siku glasi sita au nane kwa siku, kula mbogamboga na matunda, kuepuka kukaa au kusimama sehemu moja kwa muda mrefu na kufanya mazoezi.
Pia Dkt. Suzan amesema watoto wadogo wanaweza kupata bawasiri hivyo ameshauri kwa mama anayenyonyesha kuhakikisha anakula matunda, chakula cha kutosha pamoja na maji ya kutosha ili kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa huo.