Buha FM Radio

Wasiojiweza zaidi ya 200 washikwa mkono Buhigwe

June 27, 2025, 11:20 am

Baadhi ya wasiojiweza wakipokea msaada kanisani. Picha na Emily Adam.

Kwa mjibu wa mchungaji Abakuki kanisa lake limekuwa likitoa misaada hiyo kwa watu hao ili kuendelea kutimiza maandiko matakatifu ya bibilia kama yanavyosisitiza.

Na Emily Adam

Zaidi ya wananchi 200 wasiojiweza wa kijiji cha Janda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wamepokea msaada wa mavazi kutoka kanisa la Pentekosite motomoto lililopo kijijijini humo ikiwa ni sehemu ya kanisa hilo kuwasaidia wajane, wagane, wazee, walemavu na watoto ya tima.

Akikabadhi msaada huo Mchanagaji  wa kanisa hilo Ombeni Abakuki amesema kuwa vitu vilivyotolewa kwa watu hao ni mavazi, viatu, chumvi pamoja na vyombo vya kulia chakula na kuongeza kuwa watoa kwa wote bila kubagua Dhehebu wala Dini

Sauti ya Mchungaji Ombeni Abakuki.

Ameongezea kuwa kanisa hilo limekuwa likitoa zawadi hizo kwa watu hao kama utaratibu waliojiwekea ili kuwahudumia watu wasiojiweza kama maandiko ya biblia yanavyosisitiza.

Hata hivyo amewaasa viongozi wamadhebu mengine kujitokeza na kutoa msaada wa halinamali kwa watu wanye uhitaji ili kujiwekea thawabu kubwa kwa Mungu.

Sauti ya Mchungaji Ombeni Abakuki.

Kwa upande wao wanufaika wa msaada huo wamempongeza mchungaji huyo pamoja na uongozi wa kanisa hilo kwa ujumla na kuwataka kuendelea na moyo huo wa huruma wa kuendelea kuwasaidia wananchi wasiojiweza ndani na nje ya kijiji cha Janda huku wakiyataka makanisa mengine kuendelea kijitokeza na kutoa misaada ya namna hiyo.

Sauti ya baadhi ya wanufaika wa msaada huo.

Kwa mjibu wa mchungaji Abakuki kanisa lake limekuwa likitoa misaada hiyo kwa watu hao ili kuendelea kutimiza maandiko matakatifu ya bibilia kama yanavyosisitiza.