Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 27, 2025, 10:52 am

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika mkutano huu wameshukuru kwani mkutano umemalizika kwa amani lakini umewafundisha mambo mengi ikiwa pamoja na kukaa na familia na kulea watoto katika maadili mazuri yanayohitajika katika jamii.
Na Irene Charles
Katibu wa idara ya wanawake taifa katika kanisa la Babtisti Tanzania mwl. Lucy Samsoni ametoa wito kwa wanawake kumtumikia mungu kwani nafasi ya mwanamke ni kubwa sana ambayo mungu ameweka ndani yake. Amesema hayo katika mkutano wa kanda wa idara ya wanawake uliyofanyika kanda ya magharibi kata Buhoro amesema mwanamke akisimama katika nafasi yake kuanzia ngazi ya familia lazima mambo yatimie.
Kwa upande wake katibu wa kanisa la Babtisti nyamsanze kata ya Buhoro ndg. Selemani Balagwana ameushukuru umoja wa wanawake kwa kutambua pia uwepo wao na kuwakaribisha pia wanaume katika mkutano huu hata kuchangia mawazo ya kiinjili ili kujenga jamii yenye umoja.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika mkutano huu wameshukuru kwani mkutano umemalizika kwa amani lakini umewafundisha mambo mengi ikiwa pamoja na kukaa na familia na kulea watoto katika maadili mazuri yanayohitajika katika jamii.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwasaidia wanawake kujiinua kiuchumi na malezi katika familia ambapo kwa kanda ya magharibi inajumuisha mkoa wa Kigoma, Katavi na Tabora kwa mwaka 2025 umefanyika katika kanisa la Babtisti Nyamsanze Buhoro.