Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 27, 2025, 10:39 am

“Tunashukuru sana jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutupatia elimu hii kwani tumekuwa kusafirisha abilia pasipo kujua sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa katika kazi hii pia tunaahidi tuitafanyia kazi yale yote tuliyofundishwa kwenye semina hii”
Na Paulina Majaliwa
Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kunusuru maisha yao na watumiaji wa barabara kwa ujumla. Akizungumza katika shule ya sekondari Bogwe Mkuu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kasulu ACP Damas Patrick amesema kuwa baadhi ya maafisa usafirishaji hawafuati sheria za usalama barabarani jambo linaloweza kupelekea ajali.
Aidha amesema kuwa ni vyema kwa kila mtu anayetumia chombo cha moto kusafirisha abiria kuafa taratibu kwa kuwa na leseni ya udereva pamoja na leseni ya umiliki wa chombo hicho ili kuweka utaratibu mzuri vya kumiliki vyombo vya moto.
“Ukiangalia bodaboda wengi wanaendesha vyombo vyao bila leseni kwahiyo niwaombe tu kila mmoja ashughulikie maswala mazima ya leseni ili kufanya kazi kwa kujiamini Zaidi” Amesema ACP Damas
Kwa upande wake Bw. Salum Pazzy Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA, amewaomba maafisa usafirishaji hao kuanzisha chama chao cha ushirika ili kujiinua kiuchumi kwani LATRA imeweka mazingira wezeshi kwa maafisa kuanzisha vyama vya ushirika.
“Vyama vya ushirika ni moja kati ya vitu ambavyo vinaweza kuwasaidia kuwekeza au kuwa na akiba ambayo inaweza kukusaidia hapo mbelene kwahiyo nawaombeni mjiunge na vya ma vya ushirika’’. amesema Salum Pazzy
Nao baadhi ya maafisa usafirishaji kutoka wilayani Kasulu wameshukuru kwa kupatiwa elimu hiyo huku wakiuomba uongozi wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuendelea kutoa elimu kwa maafisas usafirishaji pia wameahidi kufanyia kazi yakle yote waliyofundishwa katika hafla hiyo. “Tunashukuru sana jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutupatia elimu hii kwani tumekuwa kusafirisha abilia pasipo kujua sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa katika kazi hii pia tunaahidi tuitafanyia kazi yale yote tuliyofundishwa kwenye semina hii”wamesema maafisa usafirishaji