Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 19, 2025, 10:42 pm

Mgogoro wa mpaka uliopo kati ya kata ya mwilavya na kata ya kigondo kwa sasa umesawasilishwa katika ofisi ya mkurugenzi kuhakikisha unatafutiwa suluhisho licha ya wananchi kutoshiriki mkutano wa awali utatuzi.
Na Irene Charles
Diwani wa kata ya Mwilamvya halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma Emmanuel Gamuye amesema kuwa mgogoro wa mpaka uliopo kati ya kata ya Mwilavya na kata ya Kigondo kwa sasa umesawasilishwa katika ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha unatafutiwa suluhisho licha ya wananchi kutoshiriki mkutano wa awali wa utatuzi.
Amesema hayo Juni 19, 2025 kupitia kipindi cha shangwe la asubuhi na kusema kuwa kwa sasa ana hakika mgogoro utamalizika kwa wakati kwa kuwa umefikia hatua nzuri ya usuluhishi wa mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Diwani Gamuye amesema kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 zimetolewa na Serikali katika kipindi cha miaka 5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za afya na elimu kwenye kata yake.
Katika kata ya mwilavya mikopo ya asilimia 10 ya pato la halmashauri zaidi ya shillingi milioni 72 zilitolewa na vikundi mbalimbali vilivyojitokeza kwa lengo la kujikwamua kiuchumi hasa kwa makundi maalumu kama vijana, wanawake na walemavu.
Juni 20, mwaka huu ni siku wa kuvunjwa kwa mabaraza ya madiwani kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa juni,16 huku akisisitiza kuwa baada ya kuvunjwa kwa baraza hakuna diwani yoyote atakeye ruhusiwa kufanya mkutano wowote atakaye bainika sheria itafuata zidi yake.