Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 14, 2025, 12:01 pm

Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Dkt. Innocent Mhagama amesema zoezi la kuandikisha kaya za wanufaika wa vyandarua vyenye dawa katika wilaya hiyo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo lengo la awali ilikuwa kuandikisha kaya elfu 47,467 lakini jumla ya kaya elfu 51,828 zimeandikishwa sawa na asilimia 109 ya lengo.
Na Irene Charles
Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua bila malipo ambapo zaidi ya vyandarua laki moja vimeanza kugawiwa kwa wananchi wilayani humo ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Dkt. Innocent Mhagama amesema zoezi la kuziandikisha kaya za wanufaika wa vyandarua vyenye dawa katika wilaya hiyo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo lengo la awali ilikuwa kuandikisha kaya elfu 47,467 lakini jumla ya kaya elfu 51,828 zimeandikishwa sawa na asilimia 109 ya lengo.
Akizindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa katika wilaya ya Buhigwe ambayo imefanyika katika kijiji na kata ya Mnyegera Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina ameipongeza SerikaIi kwa hatua hiyo inayolenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
Baadhi ya wananchi wa kata Mnyegera wametoa wito kwa serikali kufuatilia kaya zitakazotumia vyandarua hivyo kinyume na utaratibu huku wakiishukuru serikali kwa kuwapatia vyandarua hivyo nakueleza kuwa maambuki ya ugonjwa wa malaria yatapungua hasa kwa wanawake wajawazito na watoto.