Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 11, 2025, 2:15 pm

Denis juliasi na Abeli John wameeleza kuwa vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda mwingi katika michezo mbalimbali isyowaingizia kipato kwa kuzadharau na kuchagua kazi hasa zile zinazohitaji kutumia nguvu kwa madai kuwa wamesoma.
Na Emil Adam
Vijana wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameaswa kujikita katika shughuli halali za kuwaingizia kipato hali itakayowaepusha kuishi maisha tegemezi kutoka kwa wazazi na walezi wao pamoja na kupunguza vitendo vya wizi na ukabaji mitaani.
Hayo yamebanishwa na baadhi ya wasafirishaji wa abiria na mizigo kwa kutumia baiskeli wakati wakiongea na Buha FM Radio mjini Kasulu kuhusu njia mabalimbali za vijana kujipatia riziki zao za kila siku za kuendesha maisha yao .
Mmoja wa madereva hao Bw. Innocent Meshaki amesema kuwa baiskeli imemsadia kujipatia kipato kinacho msadia kujikimu katika maisha yake na familia kwa ujumla.
Nao madereva wengine wa baisikeli Bw. Denis juliasi na Abeli John wameeleza kuwa vijana wengi wamekuwa wakipoteza mda mwingi katika michezo mbalimbali isyowaingizia kipato kwa kuzudharau na kuchagua kazi hasa zile za kutumia nguvu kwa madai kuwa wamesoma jambo linalowafanya kuishi kwa kutegemea wazazi na walezi.
Aidha wamesema kupitia baisikeli zao kwa siku wanaingiza wasitani wa shilingi elfu tisa hadi elfu kumi na tano kulingana na mzunguko na upatikanaji wa wateja na kuongeza kuwa wakati mwingine huwa wanazulumiwa na abiria wakolofi.
Baadhi ya vijana wilayani Kasulu mkoani Kigoma wanashindwa kutimiza malengo kutokana sababu mbalimbali kama vile kutojituma pamoja na kudharau baadhi ya kazi hali inayowapelekea kuishi maisha ya kutegemea ndugu ,wazazi na walezi wao.