Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 7, 2025, 4:27 pm

Mradi wa Shule Bora waendelea kutoa mafunzo ya uwezeshaji kwa waratibu wa elimu, maendeleo ya jamii na usitawi wa afya ili kusaidia kuwabaini watoto wenye mahitaji maalumu shuleni na katika jamii na kuondokana na changamoto inayowakabili watoto wenye mahitaji maalumu shuleni.
Na: Sharifat Shinji
Halmashauri ya Mji Kasulu imeratibu mafunzo ya uwezeshaji kwa waratibu wa elimu, maendeleo ya jamii na usitawi wa afya ili kusaidia kuwabaini watoto wenye mahitaji maalumu shuleni na katika jamii ili kuwasaidia watoto wenye changamoto mbalimbali kupata haki ya kielimu.
Akizungumza jana mtoa mafunzo hayo na mwezeshaji wa kitaifa wa Shule Bora kutoka mkoani Singida Mwl. Pendo Misabo ameeleza mafunzo hayo yatawawezesha watoto wote wenye mahitaji maalumu ya kielimu kupata afua sitahiki zitakazowawezesha kushiriki na kujifunza kwa njia salama na sahihi wakati wakiwa shuleni.
Aidha kwa upande wake muwakilishi wa idara ya udhibiti ubora wa shule Halmashauri ya Mji Kasulu Ndg. Abdalla Agota amesema mafunzo haya yataibua na kubaini watoto wenye mahitaji maalumu ili kuwasaidi changamoto wanazozipitia katika elimu na mahitaji mengine.
Katika hatua nyingine Mwl. Elizabeth Malangu ambeye ni mwalimu wa wanafunzi wenye Ulemavu ameeleza namna mafunzo hayo yatakavyo wawezesha walimu pamoja na jamii namna ya kutambua na kubaini watoto wanaoishi katika mazingira ili kupata afua stahiki za kuwawezesha katika maswala ya elimu.
Mnamo March13, 2025 Taasisi ya Elimu Bora nchini ilizindua Mpango wa Programu ya Utafiti Tatuzi Kuhusu Usalama Jumuishi katika Elimu ikiwa na lengo la kuwasaidiwa watoto wote nchini wenye ulemavu na wasio na ulemavu ili kuwawezesha kupata elimu bora bila changamoto yoyote ya unyanyapaa pamoja na ukatili juu yao.
