Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 4, 2025, 9:31 pm

Baadhi ya wazazi katika Halmashauri ya Mji Kasulu wajipanga kushilikiana na walimu kulinda na kujenga madili bora kwa wanafunzi ili kuendelea na taifa lenye raia wenye madili bora.
Na: Paulina Majaliwa
Baadhi ya wazazi katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wamewaomba walimu kushirikiana na wazazi katika kuimarisha maadili na malezi ya wananfunzi wanapokuwa shuleni.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Buha FM radio ambapo wamesema kuwa shule ni moja ya sehemu ambayo mtoto anapata maadili mema na malezi mazuri hivyo wamesema ni wajibu wa wazazi na walimu katika kujenga jamii yenye maadili mema.
Aidha wamesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kuwaheshimu walimu kama wanavyo waheshimu wazazi wao wawapo majumbani kwani walimuni watu wanaowasaidia wazazi katika malezi ya Watoto ili kuimarisha maadili katika jamii.
“Tunawashukuru sana walimu wanatusaidia kuwalea watoto wetuwanapokuwa shuleni kikubwa tuwaombe wanafunzi wawe na nidhamu na wawaheshimu walimu kama wanavyotuheshimu sisi wanapokuwa nyumbani” Amesema miongoni mwa wazazi hao.
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya msingi na awali Kalinone iliyopo wilayani Kasulu Mwl.Eston Emanuel Edward amesema kuwa malezi shuleni ni miongoni mwa vipengele vinavyozingatiwa na walimu wote hivyo kila shule inaundwa na kamati ya maadili na malezi ili kuwaweka wanafunzi katika misingi inayotakiwa wawapo shuleni na hata wanapokuwa nyumbani.

Katika hatua nyingine wazazi wameomba uongozi wa shule kuwakanya baadhi ya walimu wanaojaribu kuvunja maadili yao kwani wanafunzi wanajifunza jinsi ya kuishi katika jamii kulingana na kile wanachokiona kutoka kwa walezi, pamoja na walimu wao.