Buha FM Radio
Buha FM Radio
June 4, 2025, 3:09 pm

Wakazi wa mtaa ya Kigungani kata ya Mwilamvya katika Halmashauri ya Mji Kasulu waonywa kuhudhuria misibani wakiwa wamelewa na kuanzisha fujo na kutoa maneno machafu yanayoumiza kwa wafiwa na waombolezaji katika msiba.
Na: Mbaraka Shaban
Mwenyekiti wa kamati ya maafa kata ya Mwilamvya halmashauli ya mji Kasulu mkoani Kigoma Mwl. Ignasi Ruben ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kwenda misibani wakiwa wamelewa nakusababisha vurugu kwa waombolezaji.
Akizungumza na Buha FM radio Juni 02 mwaka huu Mwenyekiti huyo wakati akitoa taarifa ya kamati ya maafa kwa wananzengo(wanajamii) wa mtaa wa Kigungani Kata ya Mwilamvya Katika halmashauri ya Mji Kasulu wakati wa kuanua matanga ya Emmanuel Ilambona Emmanuel.
“hatuhitaji watu mje msibani mkiwa mmelewa kauli hii naisemakutokana na kijana mmoja aliyekuja hapa msibani akiwa amelewa nakuanza kuongea maneno magumu kwa wafiwa na waombolezaji hivyo jambo hili sio zuri na halileti picha nzuri kwa jamii yetu” Amesema Mwl. Ruben.

Aidha mwenyekiti Ignas amewataka wakazi wa mtaa huo kuendelea kufuata sheria, taratibu na kanuni walizojiwekea katika jamii zao ili kuwa namuunganiko na ushirikiano mzuri katika vipindi vya nyakati zote za furaha na huzuni zitakazokuwa zinajitokeza katika jamii.
Kwa upande wake kijana Esau Andason aliyefika msibani hapo akiwa amelewa ameomba msamaha mbele mbele ya wananchi kwa kitendo alichokifanya mbele ya umati huo wakati watu wakiwa katika majonzi ya kupotelewa na ndugu yao na kuahidi kutorudia kufanya vurugu sehemu yeyote wala kunywa pombe tena.
“Jamani nakiri kuwa nimekosea naombeni mnisamehe kwa kufanya fujo msibani kwa kuwa nilikuwa nimelewa na sababu ya haya yote ni marafiki ninaokaa nao na kuanzia leo sinywi tena pombe” Amesema Esau.
Katika hatua nyingine Esau amewaomba vijana wenzake kuacha tabia mbaya katika jamii na kutafta marafiki sahihi ambao watakuwa na ushari mzuri na kuacha kuwapa nafasi kubwa marafiki wanaoweza kuharibu mstakabali wa maisha yao ya badae.

Unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha madhara katika mwili wa binadama hata madhara katika jamii hivyo wataaramu wa afya wanashauri kutumia pombe kwa kiasi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza katika mwili wa binadamu au jamii, Pombe inaweza kukufurahisha kwa kiasi,lakini inaweza kukuhudhunisha endapo ikitumika vibaya.