Buha FM Radio

Ufinyu eneo la soko kuu la mazao Kasulu wasababisha ajali

June 4, 2025, 10:46 am

Gari aina ya Probox lenye namba za usajili T-948 DNS mali ya Bw.Paul Makelemo lililosabaisha ajari katika eneo la soko kuu la mazao Mnadani Kasulu Mjini. Picha na Emily Adam.

Mashuuda wa tukio la ajari katika eneo la soko kuu la mazao wilayani kasulu na wametaja sababu zilizopelekea ajarihiyo kutokea katika eneo hilo.

Na: Emily Adam

Mwanaume anayejulikana kwa jina la Erick Wanguwangu amejeruhiwa baada ya kuongwa na gari aina ya Probox lenye namba za usajili T-948 DNS mali ya Bw.Paul Makelemo lililokuwa likiendeshwa na Rewis Telifol katika eneo la soko la kuu la mazao Mnadani wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Tukio hilo limetokea jana majira ya mchana ambapo mashuda wa ajari hiyo wamesema chanzo ni dereva wa gari hilo kutochuwa tahadhari wakati akiendesha kwenye eneo hilo lililokuwa na msongamano mkubwa wa magari makubwa ya kubeba mizigo pamoja na msongamano wa watu.

Mashuda wa tukio wakielezea namna ajari ilivyotokea katika eneo hilo.

Mkaguzi wa magari kutoka jeshi la polisi wilayani Kasulu Koplo Fadhili Ndege amefika katika eneo la tukio na kuamuru dereva pamoja na gari hilo kupelekwa katika kituo cha polisi kwaajili ya mahojiano zaidi.

Mkaguzi wa magari kutoka jeshi la polisi wilayani Kasulu Koplo Fadhili Ndege akifanya ukaguzi wa gari lililosababisha ajari katika eneo hilo la mnadani. Picha na Emily Adam.

Hata hivyo amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini pamoja na kuachanana tabia ya kutumia vileo wakati wakiwa katika shughuli zao za usafirishaji wa abiria na mizigo ili kulinda usalama wao na watu wengine wakiwemo watembea kwa miguu.

Koplo Fadhili Ndege akizungumzia namna madereva wanavyotakiwa kufuata sheria wanapokuwa na vyombo vya moto.

Kulingana na ufinyu wa soko la kuu la mazao Mnadani wilayani Kasulu kumekuwa na msongamano wa magari ya mizigo pamoja na eneo dogo la kufanyia shughuli za uuzaji na ununuzi wa mazao mbalimbali kama Mahindi, Maharage Mihogo na mazao mengine hupelekea changamoto mbaribari ambazo wakati mwingine husababisha migogoro baina yao.

Gari aina ya Probox lenye namba za usajili T-948 DNS mali ya Bw.Paul Makelemo lililosabaisha ajari katika eneo la soko kuu la mazao Mnadani Kasulu Mjini. Picha na Emily Adam.