Buha FM Radio

Viongozi wa dini Kasulu waombwa kuhubiri amani kuelekea uchaguzi

June 4, 2025, 12:24 pm

Pichani ni baadhi ya viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa katika kongamano la harambee ya kuchangia ununuzi wa gari la kwaya ya Kasulu Cathedral  Choir KCC. Picha na Emily Adam.

Viongozi wa dini wilayani Kasulu waombwa kuendelea kuhubiri amani na kuliombea taifa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Na: Emily Adam

Viongozi wadini wilayani kasulu mkoani kigoma wameombwa kuendelea kuhubiri amani  pamoja na kuliombea taifa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuepuka malumbano na migogoro ndani ya jamii.

Ombi hilo limetolewa Juni mosi mwaka huu na mwenyekiti wa Chama cha Mapainduzi  CCM Wilaya ya Kasulu Bw.Mbelwa  Abdallah  wakati akizungumza kwenye kongamano la harambee ya kuchangia ununuzi wa basi dogo aina ya Tata la kwaya ya Kasulu Cathedral  Choir KCC iliyofanyika katika Kanisa la Angilikana Kasulu mjini.

Aidha Mbelwa amesema kuwa Maasikofu, Mapadri na Mashekhe pamoja na watumishi wote wa Mungu wanapaswa kuliombea taifa na kuwaasa waumini wao kuzidi kuitunza  na kuiendeleza amani ya Tanzania wakati na baada ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapainduzi  CCM Wilaya ya Kasulu Bw.Mbelwa  Abdallah akizungumza katika kongamano la harambee.

Katika harambee hiyo viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na waumini wamechangia kulinganana kipato chao huku mgeni rasmi wa harambee hiyo Bw.Dubai Evacy Chocha ambaye ni mfanya biashara katika Mji wa Kasulu na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Kasulu amewahimiza watu wote waliokuwepo katika kongamano kuendelea kuchangia ili kukamilisha zoezi la ununuzi wa basi hilo.  

Sauti ya Dubai Chocha mgeni rasmi wa shughuli ya uchangia wa pesa kwa ajili ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kasulu Cathedral  Choir KCC.

Kwa upande wake askofu wa Diocese ya Western Tanganyika Emmanuel Charles Mbwata amewapongeza viongozi wa serikali, wanakwaya wa KCC na waumini wote waliojitokeza kuchangia kwenye harambee hiyo huku akiwaasa wote waliotoa ahadi kuhakikisha wanaitekeleza kwa wakati nakuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuhamasisha swala la amani na utulivu kwa waumin iwao linaendelea kuwepo na kwa wananchi wote.

Sauti ya Askofu wa Dioces ya Western Tanganyika Emmanuel Charles Mbwata.

Kwaya ya KCC inauhitaji wa jumla ya shilingi milioni 150/= kwa ajili ya ununuzi wa gari litalowasaidia kuarhisisha kuendelea kutoa huduma ya kuinjilisha kwa njia ya nyimbo katika maeneo yote yaliyopo jirani na Wilaya ya Kasulu sanjari na nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki.