Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 20, 2025, 5:50 pm

“Kwa mwaka huu tutaendelea kufata vigezo kama ilivyokuwa mwaka jana tutazindua miradi ya afya, Miradi ya elimu, miradi ya Barabara, miradi ya maji na miradi ya mapato ya ndani itakuwemo” Amesema Daudi Stinga.
Na: Sharifat Shinji
Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma, imejipanga kutekeleza uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Serikali katika kampeni ya Mbio za Mwenge wa Kitaifa zinazotarajiwa kuanza itakapofika Septemba mwaka huu.
Akizungumza na Buha Fm Radio leo Baada Kikao cha maandalizi ya Mbio za Mwenge Mratibu wa zoezi hilo Ndg. Daudi Stinga amesema halmashauri ya Mji Kasulu imejipanga kufanya vizuri katika zoezi hilo ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa mwaka 2024.

Aidha Stinga amesema mwaka huu watazindua miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, Barabara, maji Pamoja na miradi ya mapato ya ndani huku akiwaomba wadau kuonga mkono jitihada za serikali katika kutekeleza miradi katika kukuza Uchumi wa nchi.
Katika hatua nyingine Mwl. Zawadi Mnana ambaye ni mjumbe wa Mbio za Mwenge 2025 amesema mwaka huu wameanza mapema kujiandaa ili kubakia katika nafasi ya kwanza na nafasi za juu zaidi kitaifa.
Kwa upande wake Mwl. Michael Benezeth ambaye ni Mwenyekiti wawakuu wa shule katika halmashauri ya Mji Kasulu amesema maandalizi yameanza mapema ili wajumbe wapate kupendekeza maeneo ambayo yanauhitaji ya kufikiwa na Mwenge wa kitaifa.
Halmashauri ya Mji Kasulu kwa mwaka 2024 katika zoezi la mbio za mwenge ilishika nafasi ya kwanza kati ya halmashauri nane za mkoa wa Kigoma na kushika nafasi ya 46 kitaifa hivyo mwaka huu wadau wa maendeleo ya mbio za Mwenge wamejipanga kushika nafasi za juu zaidi kitaifa ili kuipa hadhi halimashauri na mkoa kwa ujumla.
