Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 19, 2025, 7:37 pm

Jamii yashauriwa kufuata na kutumia njia za uzazi wa mpango ili kupunguza utapiamlo unaoweza kujitokeza kutokana na familia nyingi kujifungua bila kufuata njia za uzazi wa mpango.
Na: Kudra Mbali
Wananchi katika halmashauri ya Mji Kasulu wameshauriwa kufuata na kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuondokana na madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na kujifungua bila mpangilio hali ambayo inaweza kupelekea wazazi kushindwa kutunza na kulea familia zao.
Akizungumza na Buha FM radio muuguzi kutoka zahanati ya Nyumbigwa katika Halmashauri ya Mji Kasulu Bi. Beatrice Machibya Mei 19 mwaka huu na kubainisha athari ambazo mzazi anaweza kuzipata kutokana na kuendelea kujifungua bila kufata mpangilio wa uzazi.
Aidha Bi. Machibya amesema uzazi wa mpango ukifuatwa kwa usahihi utaleta faraja katika familia kwani huwawezesha wanafamilia kuwa na muda wa kutosha katika kufanya kazi za maendeleo kuliko wale wanaoishi bila kufuata mpangilio wa uzazi.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi katika Halmashauri ya Mji Kasulu wameeleza namna wanavyoelewa kuhusu mpango wa uzazi katika familia huku wengine wakitaja faida za kufuata mpangilio wa uzazi katika ndoa na familia.
Kwa muuji wa shirika la takwimu Tanzania NBC mwaka 2022 lilichapisha takwimua zinazoonesha asilimia 38 ya wanawake walioolewa wanatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango, ikijumuisha asilimia 31 ya wanaotumia njia zozote za kisasa na asilimia 7 ya wanawake wanaotumia njia za asili za uzazi wa mpango.
