Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 17, 2025, 8:33 pm

Serikali katika Halmashauri ya Mji kasulu mkoani Kigoma imeahidi kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara za mitaa kwa kiwango cha lami ili kulahisisha shughulii za usafirishaji zinazofanyika katika Mji huo.
Na: Mbaraka Shabani
Halmashauri ya Mji kasulu mkoani Kigoma imepanga kutengeza na kuboresha barabara za mitaa katika kata zote zilizopo ndani ya halimashauri hiyo kwa kiwango cha lami ili kulahisisha shughuli za usafirishaji.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmasauri ya mji Kasulu Bw.Norah Noel wakati akizungumza na Buha Fm radio juu ya mchakato wa zoezi la kurekebisha barabara hizo pamoja na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na serikali wilayani humo.

Aidha Noel ameongeza kwa kusema baadhi ya barabara zitajengwa na serikali huku nyingine kutekelezwa na shirika la maendeleo la kimataifa UNDP hali ambayo itaufanya mji wa kasulu kufunguka kibiashara kitu ambacho amewasa wakazi wa mji huo kuchangamkia fursa za ajira zitakazokuwa sinatolewa na wakandarasi wa shughuli hiyo ya ujenzi.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mwl.Dismas Mbee Msafu amepongeza juhudi za serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya Barabara huku akiwataka TARURA kutengeneza mifereji ya maji ili kuepuka ufalibifu unaojitokeza kila inaponyesha mvua na maji kuelekea barabarani.
Halmashauri ya Mji Kasulu Barabara nyibgi za mtaa zinakabiliwa na mashimo yaliyosababishwa na mvua za msimu hivyo serikali imedhamilia kutekeleza ujenzi wa Barabara katika maeneo yote ya Mji huo lengo nikuboresha sekta ya usafirishaji na kuupa hadhi mji wa Kasulu na kuweka katika mpangilio bora wa kuvutia.
