Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 9, 2025, 1:26 am

“Vitabu vya ziada na kiada vitawasaidia wanfunzi kuongeza maalifa na weledi na vitawasaidia kuelewa na kujifunza mambo mengi kuliko kusubili mwalimu aje akufundishe darasani hivyo wakisoma vitabu ya kiada vitaongeza ufaulu katika masomo yao”Amesema Mwl.Edward Kasabuku.
Na: Emily Adam
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kusoma kwa bidii vitabu vya ziada na kiada ili kuongeza maarifa na weledi utakaowasaidia kufanya vizuri katika mitihani yao.
Wito huo umetolewa na Mwalimu wa taaluma katika shule ya sekondari Mwilamvya Mwl.Edward Kasabuku wakati akizungumza na Buha fm radio juu ya jitahada mbalimbali zinazoweza kusaidia kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Aidha Mwl.Kasabuku amewahimiza wazazi na walezi wilayani kasulu kuwapeleka watoto wao shuleni kwani elimu ndio urithi pekee usio filisika kwa mtoto pamoja na kujenga tabia ya kufuatilia maendeleo ya kimasomo kwa watoto wao.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema wanaendelea kutumia muda wao wa ziada kijisomea kwa njia ya majadiliano huku wakiwatumia walimu wao kwa pale ambapo wanashindwa kuelewa.
Baadhi ya wanafunzi katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri hasa katika mitihani yao ya mwisho kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu,miundombinu mibovu,utoro pamoja na uhaba wa vitabu vya zida na kiada mashuleni.
