Buha FM Radio

Wananchi waombwa kulipia bili za maji kwa wakati

May 8, 2025, 3:31 pm

Picha ni bomba la maji katika moja ya makazi ya wakazi wa Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Emily Adam.

Mamlaka ya maji safi na salama katika Halmashauri ya Mji Kasulu yaombwa kuboresha huduma ya maji katika baadhi ya maeneo yanayotoa maji machafu ili kuwa na mwendelezo wa utoaji maji safi kwa jamii.

Na: Emily Adam

Watumiaji wa maji katika Halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kulipa bili zao za maji kwa wakati ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiopungua shilingi elfu kumi.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa mamlaka ya usambazaji maji usafi na mazingira katika  Halmashauri ya mji kasulu mhandisi Goodluck Somwe wakati akizungumzia hali utumiaji na upatikanaji wa maji safi miongoni mwa wakazi wa mji huo.

Sauti ya mhandisi Goodluck Somwe 01.

Aidha mhandisi Somwe ameeleza  kuwa wanaendelea na zoezi la kusambaza mtandao wa bomba kwa maeneo ambayo hayana huduma hiyo ya maji ili kurahisisha uapikanaji wa huduma ya maji katika meneo mengi ya makazi ya watu.

Sauti ya mhandisi Goodluck Somwe 02.

Kwa upande wao baadhi wananchi katika halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wameiomba mamlaka hiyo kuhakakikisha inaboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo  baadhi ya maeneo wanalazimika kutumia maji yasiyo salama.

Sauti za baadhi ya wananchi.

Akifafanua juu ya swala la mabomba kutoa majimachafu mhandisi Somwe amewomba wakazi hao kuwa wavumilivu na kusema  swala hilo linaendea kufanyiwa ufumbuzi kwa kujenga machujio katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmasahauri ya mji Kasulu.

Sauti ya mhandisi Goodluck Somwe 03.

Matumizi ya maji majumbani katika Halmashauri ya Mji Kasulu wanalipa Tsh.300/= kwa unit moja  sawa na lita 1000 huku taasisi zote za umma na binafisi hulipa Tsh. 400/= kwa kila Unit moja.