Buha FM Radio

Baptist ataja manufaa ya redio za kijamii

April 24, 2025, 11:40 pm

Pichani ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Kijamii Tanzania (TADIO) Ndg. Baptist John. Picha na Amua Rushita

Baptist ameeleza faida za mtandao wa redio za kijamii zinavyonufaisha vituo vya redio na wafanyakazi wake.

Na Sharifat Shinji

Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Kijamii Tanzania (TADIO) Ndg. Baptist John amewataka wanachama wa redio za kijamii nchini kuendelea kufanya vizuri ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuchapisha maudhui bora katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ameyasema hayo Aprili 24 wakati alipotembelea mafunzo kwa waandishi wa habari za kijamii yaliyoendeshwa na radio Tadio kwa siku mbili katika ukumbi wa Lastanar Hotel jijini Dodoma na kuwasisitiza washiriki kuyatumia mafunzo hayo katika kutangaza vyombo vyao.

Sauti ya mwenyekiti wa TADIO Ndg. Baptist John.

Aidha Baptist ameongezea kwa kusema umuhimu wa kuwa katika mtandao wa redio za kijamii ni pamoja na kusaidia kuongeza wateja na kumwezesha mwandishi kushiliki katika majukwaa mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa TADIO Ndg. Baptist John

Mafunzo ya wanahabari kuhusu matumizi ya mtandao wa redio za kijamii yamefanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia Aprili 23 na Aprili 24 yakiwa yamejumuisha wanachama wapya kutoka Buha FM Radio kutoka Kasulu Kigoma, Viwawa FM kutoka Songwe, Kagera Community Radio kutoka Kagera, Butiama FM Radio kutoka Mara na Bunda FM Radio kutoka Mara kwa lengo la kupanua wigo wa uzalishaji wa maudhui yanayolenga na kunufaisha jamii husika.

Mwenyekiti wa redio za kijamii Tanzania (TADIO) Ndg. Baptist John akizungumza na wanufaika wa mafunzo hayo. Picha na Amua Rushita