Smile FM Radio
Smile FM Radio
March 19, 2026, 10:53 am

Mamlaka ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU Mkoa wa Manyara imefuturisha watoto wenye uhitaji pamoja na wadau mbalimbali.
Na Linda Moseka
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ametoa pongezi kwa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Manyara kwa kufanya matendo ya huruma kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhan na kwaresma .
Ametoa pongezi hizo Machi 18 ,2026 katika ukumbi wa Kisora Hall wakati wa iftar iliyoandaliwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU na kuhudhuriwa na watumishi wa serikali, viongozi wa dini pamoja na wadau mbalimbali.
Kaganda amesema kuwa chombo hicho hakikuundwa kwaajili ya kutishia wananchi, wala kutengeneza hofu bali chombo hicho kimeundwa kwaajili ya kuweza kusaidia na kuharakisha maendeleo.
Aidha mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema lengo la taasisi hiyo kufanya hivyo ni ili jamii inyooke kimaadili kwani kwa kufanya hivyo jamii itakua na amani ,pia katika ibara ya 8 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ndogo ya 3 inasema moja ya jukumu kubwa la serikali ni ustawi wa jamii ,na ustawi wa watu wake.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha HOSSANA HOME CARE FOUNDATION Neema Munisi ametoa shukurani kwa TAKUKURU kwa kuona vyema kuwaalika watoto yatima kushiriki kwa pamoja IFTAR hiyo pamoja na kutoa msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu kwaajili ya watoto hao.
Doreen Dastan na Shedrack Amos kutoka kituo hicho nao wameshukuru na kuomba misaada hiyo iyendelee kutolewa kwa miezi mingine isiwe tu kwenye kipindi cha mfungo.
