Smile FM Radio
Smile FM Radio
March 2, 2026, 8:36 am

Amewataka watumishi wa serikali kutimiza majukumu yao alipokuwa wilaya ya Babati Mkoani Manyara
Na Mbaraka Sungi
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa hatosita kuwa mkali na kuchukua hatua kali dhidi ya wezi, wavivu na wale wanaodhulumu watanzania kwa hofu kuwa atachukiwa.
Ameyasema hayo leo Machi 1, 2026 akiwa kwenye ziara Babati mkoani Manyara na kueleza kuwa hagombei umaarufu wala hahitaji kupendwa wala bali kufanya kazi aliyopewa kwa usahihi na kuwasaidia watanzania.