Smile FM Radio

Kocha Matano amlipua kipa mechi na Yanga

April 26, 2025, 9:26 am

Katika picha kushoto ni kipa wa Fountain Gate John Nobo na kulia ni kocha wake Matano. Picha na Azam Media

Baada ya fountain gate kufungwa magoli manne bila na Young African kocha mkuu wa club hiyo amesema hatompanga kwenye kikosi chake golikipa wake John Nobo

Na Mbaraka Sungi

Hii ni ripoti ya kamati ya michezo kupitia Smile FM 95.3 na leo tumeangazia mchezo wa jana tarehe 21 April 2025 kati ya wenyeji Fountain Gate dhidi ya Dar Young Africans mchezo ulioanza majira ya saa kumi jioni huku ukimalizika kwa ushindi wa mabao manne kwa Yanga na huku wenyeji Fountain Gate wakiambulia patupu licha ya kuwa nyumbani.

Makocha wote wa timu zote mbili walikuwa naya kusema baada ya mchezo huo huku kocha wa fountain gate akidai kuwa kuna uwezekano mkubwa goli kipa wake wameuza mchezo na kudai kuwa golikipa wake namba moja “JOHN NOBO” hatohusika katika vikosi vinavyo fuata katika michezo yao mitatu iliyosalia na moja ya mchezo ukiwa ni wao dhidi ya Azam fc ambao utachezwa katika kiwanja cha Tanzanite kwaraa.

Sauti ya kocha wa Fountain gate Robert Matano

Kwa upande wa kocha wa yanga yeye licha ya ushindi wa mabao manne alisema kuwa mchezo haukuwa rahisi hasa kipindi cha kwanza na kuishia kuwashukru wachezaji wote wa yanga na mashabiki kwa ujumla.

Sauti ya Kocha wa Young Africans Miloud Hamdi