Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
September 29, 2025, 5:50 pm

Wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani Muleba wameaswa kutekeleza wajibu wao wa ulipaji kodi, pamoja na kutumia mashine za kielektroniki ili kulipa kodi sahihi kwa mamlaka ya mapato nchini TRA.
Na Anold Deogratias
Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA wilaya ya Muleba mkoani Kagera, imewakumbusha wamiliki wa nyumba za kulala wageni kutekeleza wajibu wao wa ulipaji kodi, ikiwemo usajili, uwasilishaji na usahihi wa ritani, pamoja na kufanya malipo kwa wakati.
Woto huo umetolewa na meneja wa TRA Muleba, William Mneney, wakati wa semina iliyowakutanisha wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani humo ambapo amewakumbusha wamiliki wa nyumba hizo kuhakikisha wanalipa tozo ya kitanda kwa wakati ili kuongeza mapato ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Sauti ya meneja wa TRA Muleba, William Mneney

Pia Mneney amewataka wamiliki hao kutumia mashine za kielektroniki na kutoa risiti kwa kila huduma wanayotoa, akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza uwajibikaji katika biashara zao.
Sauti ya meneja wa TRA Muleba, William Mneney
Kwa upande wao washiriki wameeleza kuwa wameelimika kuhusu umuhimu wa kutekeleza wajibu wao, hususan matumizi ya risiti za kielektroniki ili kuongeza ufanisi na uwazi katika ulipaji kodi.
Sauti ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani Muleba.

