Kagera Community Radio

Fabius aahidi kukamilika kwa miradi iliyokwama Igurwa

September 5, 2025, 3:25 pm

Fabius Clavery mgombea udiwani kata Igurwa

Kufuatia kukwama kwa baadhi ya miradi yamaendeleo kwa muda mrefu katika kata ya Igurwa wilayani Karagwe mgombea udiwani kupitia chama cha ACT Wazalendo ameahaidi kukamilika kwa miradi hiyo kwa muda mfupi endapo atachaguliwa.

Na Anold Deogratias

Mgombea udiwani kata ya Igurwa iliyopo wilayani Karagwe mkoani Kagera kupitia chama cha ACT Wazalendo Bw.Fabius Boniventure Clavery ameahidi kukamilisha miradi yote iliyokwama katani humo ikiwemo Ile iliyoanzishwa kwa nguvu ya wananchi, endapo atapewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari Bw.Clavery amesema kuna miradi kama Zahanati, shule za msingi,miradi ya maji na umeme ambayo imekwama kwa muda mrefu sasa hivyo kata hiyo inahitaji mtu mwenye weledi wa kuisemea na kuwasemea wananchi ili ikamikishwe na ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Faibius Clavery

Aidha mgombea huyo amewaahidi wananchi wa kata hiyo kila kitongoji kupata umeme ili kukuza uchimi wa mwananchi mmoja mmoja kupitia shughuli za kibiashara.

Fabius Clavery mgombea udiwani kata Igurwa

Kuhusu miundombinu ya barabara, Fabius ameahidi kutengenezwa kwa barabara za kata hiyo ikiwemo ya Omukigando-Igurwa ambayo imekuwa korofi hivyo kurudisha nyuma shughuli za usafiri na safirishaji katika kata hiyo, pamoja na kupunguza mlima katika eneo la Omkisanje ambao umekuwa ukisababisha ajali nyingi.

Sauti ya Faibius Clavery

Pia mgombea huyo kupitia ACT Wazalendo amewaahidi vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuwatafutia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo, lakini pia kuhakikisha mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri inawafikia walengwa bila ubaguzi.

Sanjali na hayo amewaahidi wananchi wa kata ya Igurwa utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo ipo katika kata hiyo ila kutunza Amani na utulivu wa Igurwa, ikiwa ni pamoja na kutumika zaidi kama mwakilishi wa wananchi kuliko kutumikiwa.