Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
September 1, 2025, 6:23 pm

Wananchi na wamiliki wa maduka wilayani Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kufanya usafi wa jumla kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kutunza taswira nzuri ya wilaya hiyo.
Na Avitus Kyaruzi
Mkuu wa wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera Erasto Sima, amewataka wananchi na wamiliki wa maduka wilayani humo kufanya usafi wa jumla kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuepukana na magonjwa na kuuweka mji katika hali ya usafi.

DC.Siima amesema hayo alipo ambatana na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Ndg. Jacob S. Nkwera na kamati ya usalama ya wilaya na kuungana na wananchi wa kata ya Bilele manispaa ya Bukoba, katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa usafi wa jumamosi ya mwisho wa kila mwezi.
Mhe. Sima amewataka wananchi kuendeleza mshikamano na ushirikiano katika kuhakikisha mji wa Bukoba unakuwa safi na salama kwa afya ya jamiiĀ na kwamba usafi wa mazingira ni wajibu wa kila mmoja na ni msingi wa kujikinga na magonjwa ya milipuko.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ya Bukoba amewataka wakala wa barabara mjini na vijiji TARURA, na wakala wa barabara nchini TANROADS kuhakikisha wanaifanyia usafi mitaro ya kupitisha maji iyopo pembezoni mwa barabara ambayo imefunikwa.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wamepongeza uongozi wa wilaya na Halmashauri kwa kuungana nao bega kwa bega na kuonesha mfano wa vitendo katika masuala ya kijamii.
