Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
August 23, 2025, 2:13 pm

Katika kurahisisha shughuli za uokoaji na kuzima moto, viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wameshauriwa kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo yao.
Na Anold Deogratias
Viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji mkoani Kagera wametakiwa kuboresha miundombinu ya barabara za maeneo yao ili kuraisisha utoaji wa huduma za uokoaji na kuzima moto pindi yanapotokea.
Wito huo umetolewa na mkaguzi wa Jeshi la Zima moto na uokoaji mkoa Kagera, Karata Ramadhani mara baada ya zoezi la kuzima moto katika moja ya nyumba iliyopo kijiji Butairuka kata ya Maruku halmashauri ya Bukoba, ambapo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo, ingawa hakuna majerui wala kifo bali mali tu ndizo zimeungulia ndani.

Kamanda Ramadhani amewataka viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji kuboresha barabara za maeneo yao kwani walipata wakati mgumu kufika eneo la tukio kwa wakati kutokana na ubovu wa barabara.
Sauti ya mkaguzi wa Jeshi la Zima moto na uokoaji mkoa Kagera, Karata Ramadhani
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto ulianza ghafla na kusababisha taharuki kwa majirani ambao walikimbilia kutoa msaada huku wakiwasiliana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera ambao walifika kwa haraka na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujasambaa nyumba nzima.
Sauti ya mashuhuda

Nao wammiliki wa nyumba hiyo Bwa.Wiliatusi Ndibaza na Agnes Wiliatus wamesema kuwa walipata taarifa wakiwa kwenye majukumu yao na kwamba vitu vingi vimeungulia ndani ya nyumba na kuomba wasamalia wema kuendelea kuwasaidia vitu ikiwemo nguo.
Sauti ya wammiliki wa nyumba
Serikali ya kijiji hicho imeahidi kutoa msaada wa awali na kushirikiana na taasisi nyingine kuisaidia familia hiyo.
