Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
July 24, 2025, 9:25 pm

Miradi mikubwa minne inatarajiwa kujengwa katika manispaa ya Bukoaba mkoani Kagera kwa shilingi bilioni 40.2, hali itakayochochea ukuaji wa mji huo kutokana na uhitaji wa miradi hiyo kwa muda mrefu.
Na Anold Deogratias
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, imetia saini mikataba minne ya ujenzi wa miradi mikubwa ya stendi ya mabasi, soko kuu, kingo za mto kanoni na barabara kilometa 10.7 kwa thamani ya shilingi bilioni 40.2 kwa ufadhili wa benki ya dunia kupitia mradi wa TACTICS.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba hiyo RC wa Kagera hajjat Fatma Mwassa, amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi wa manispaa ya Bukoba pamoja na kupendezesha mji na kuwataka wakandasi watakao tekeleza miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Kagera amewataka wananchi wa manispaa ya Bukoba pamoja na mkoa wa Kagera kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa wakandarasi na kuwa walinzi miradi hiyo wakati wa utekelezaji wake.

Awali akisoma taarifa ya miradi hiyo meneja wa wakala barabara mjini na vijiji TARURA wilaya ya Bukoba mhandisi Emmanuel Festo Yohana, ameeleza kuwa miradi hiyo imegawanyika katika makundi mawili stendi ya mabasi na soko kuu vitajengwa kwa shilingi bilioni 18.95 na ujenzi wa Barabara na taa za Barabarani pamoja na kingo za mto kanoni kwa shilingi bilioni 21.29.
Sauti meneja wa TARURA wilaya ya Bukoba mhandisi Emmanuel Yohana
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato, amesema miradi hiyo imekuwa ni hitaji kubwa la wananchi wa manispaa ya Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla kwani inatarajia kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.

Miradi hiyo inatarajia kutekelezwa kwa muda wa miezi 15 ambapo inatarajiwa kukamilika na mwezi October 2026 na inatekelezwa na wakandasi wawili, Shaldon Liquid Campan LTD, kutoka nchini china, Dimoto Glass Lilvov atakayejenga soko kuu na stendi ya mabasi Kyakailabwa.