Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
July 10, 2025, 3:21 pm

Wananchi mkoani Kagera wameshauri kugeukia kilimo cha parachichi hasi ili kukuza uchumi wao na mkoa wa Kagera kwa ujumla

Na.Anold Deogratias
Wananchi mkoani Kagera wameshauriwa kugeukia kilimo cha parachichi hasi ili kujiinua kiuchumi kupitia zao hilo kuliko kutegemea kilimo cha kahawa na ndizi pekee.
Wito huo umetolewa na katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali watu Bw.Bwai Masahuri Biseko, aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjati Fatma Mwassa katika hafla ya uzinduzi wa shamba la parachichi hasi lilipo kijiji cha Muyenje kata Kagoma wilayani Muleba.

Amesema zao la parachichi ni moja ya kilimo cha mkakati kinachopewa kipaumbele na uongozi wa mkoa wa Kagera ambao unahamasisha kila mwananchi kupanda angalu miche 5 ya parachichi ili kujiinua kiuchumi.
Sauti ya Bwai Masahuri Biseko katibu tawala msaidizi utawala na rasilimali watu
Awali akisoma risala Bw.Mike Nshangeki, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Bukoba Investment Group (BIG) ambao ndio wamiliki wa shamba hilo, amesema kwa sasa wameendeleza hekari 75 za kilimo cha parachichi hasi kwa gharama ya shilingi milioni 296.
Sauti ya Mike Nshangeki
Nao baadhi ya wakulima wa zao hilo walioshiriki katika uzinduzi huo akiwemo Habibu Yahya Byemele, Elieth Thadeo na Nathuman Salm wamesema kuwa wanachangamoto ya kupata elimu sahihi juu ya zao hilo pamoja uhaba wa masoko pindi mazao yanapokomaa.
Sauti ya wakulima wa zao la parachichi
Mpaka sasa mkoa wa Kagera una wakuliama wa zao la parachichi 1,425 ambao udhalisha tani 9,800 za parachichi huku wilaya ya Ngara ikizalisha tani 5,000 na kuingiza zaidi ya shilingi milioni 600 kutokana na mauzo ya zao hilo.
