Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
July 5, 2025, 1:15 pm

Picha ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera Brasius Chatanda
Polisi mkoani kagera wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na baadhi ya viungo vinavyosadikika kuwa vya binadamu
Na Elisa Kapaya
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na viungo vinavyohisiwa kuwa ni vya binadamu katika nyumba moja ya wageni iliyopo Kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema watuhumiwa hao ni Piason Mdolo (42) anayejishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji wilayani Mbozi Mkoani Songwe na Randan Mlomo (64) ambaye ni mtumishi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Kamanda Chatanda ametaja baadhi ya viungo walivyokutwa navyo watuhumiwa hao kuwa ni mfupa wa taya la binadamu, kipande cha moyo wa binadamu, kipande cha sehemu za siri za mwanamke, kondo la nyuma la uzazi pamoja na ngozi za nyoka.
…………………sauti chatanda……….
Hata hivyo amesema jeshi la polisi mkoani Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani.
Kwa upande wake katibu wa shirikisho la vyama vya tiba asili mkoani kagera bwana DidaS Ngemera amesema waganga wanaopiga ramri chonganishi ndio wanaosababisha baadhi ya wananchi kujichukulia sharia mkononi ikiwemo kufanya mauaji hivyo kuomba serikali kuwachukulia hatua kali.
…….Sauti ya Didas Ngemera……..