Kagera Community Radio

Serikali yaombwa kuingilia kati kunusuru zao la kahawa

June 30, 2025, 12:08 pm

picha ya zao la kahawa ambalo ni miongoni mwa mawazo ya biashara mkoani kagera

Serikali imeombwa kuingilia kati ili kuona namna ya kuwasaidia wakulima ili kuondoa changamoto ya kahawa kutonunuliwa mnadani

Na Elisa Kapaya

MISSENYI.

Serikali imeombwa kuingilia kati suala la kahawa kutonunuliwa katika baadhi ya maeneo wilayani Missenyi mkoani Kagera ili kuona namna nzuri zaidi ya kuzungumza na makampuni yanayonunua zao hilo ili wachukue kahawa zote za wakulima.

Respicius John mwenyekiti wa chama cha msingi Nsunga

Akizungumza katika mahojiano maalum na KCR FM kuhusu hali ya msimu wa ununuzi wa zao hilo mwenyekiti wa chama cha msingi Nsunga na mkuima wa zao hilo bwana Respicius John amesema kahawa nyingi ambazo hazinunuliwi ni aina ya Robusta za maganda kiasi cha wakulima kupata hofu kutokana na baadhi ya vyama kukusanya kahawa tangu mwezi wa tano mpaka sasa hazijanunuliwa.

sauti ya Respicius John

Aidha bwana Respicius ameomba serikaLi kuendelea kusimamia suala la bei ya kahawa ambapo amesema hata kama bei elekezi itashuka lakini isiwe ya kumumiza mkulima kutokana na wakulima wengi kuzoea kuuza kwa gharama ya shilingi elfu tano kwa kilo katika minada mbali mbali.

Sauti ya Respicius John

Moja ya sababu ambazo zimakua zikitajwa kusababisha kahawa kuporomoka bei ni pamoja kushuka bei katika soko la dunia ambako kumechangiwa ba baadhi ya nchi wazalishaji wakubwa wa kahawa duniani kuongeza uzalishaji wa zao hilo.