Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
June 28, 2025, 5:04 pm

Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wilayani Muleba mkoani Kagera wametakiwa kutumia ipasavyo baiskeli walizopatiwa kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU).
Na.Avitusi Kyaruzi
Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Dkt. Abel Nyamahanga amekabidhi baiskeli 69 kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambao ni wafuatiliaji wa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo ikiwa ni ufadhili kutoka shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na uboreshaji wa huduma ya fya kwa umma (MDH) kwa shirikiana na Buffalo bicycles Tanzania, Dkt Nyamahanga amewataka wahudumu hao kutumia baiskeli hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt.Abeli Nyamahanga
Aidha mkuu huyo wa wilaya amesisitiza kuwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kazi wanayofanya ni kubwa na nzuri hivyo wanatakiwa kuendelea kujituma na kujitoa kwa ajili ya watu wanaoishi na maambuki ya virusi vya UKIMWI ili wasijione kama wametengwa bali wajisikie kama sehemu ya jamii.

Akiongea kwa niaba ya mkurungenzi wa MDH, Dkt. Irene Lema amesema katika mkoa wa Kagera wameleta baiskeli 316 na kati ya baiskeli hizo 69 wamezileta katika wilaya ya Muleba, na kwamba baiskeli hizo zitakuwa ni chachu kwa wahudumu hao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwafatilia na kutoa huduma kwa walengwa.
Sauti ya Dkt. Irene Lema mwakilishi wa mkurugenzi wa MDH
Kwa upande wao baadhi ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wilayani Muleba, Adivera Robert Ansen Kajuna Marco, na wameishukuru serikali kwa kuendelea kushirikaina na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya na kuweka mazingira rafiki yanayosaidia wadau kutoa michango inayoigusa jamii.
Sauti ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wilayani Muleba
