Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
June 23, 2025, 5:45 pm

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imesaini mkataba wa ujenzi wa soko la Bunazi katika kata ya Kassambya utakaogharimu shilingi billion 17.5, unaotarajiwa kukuza uchumi wa mwananchi mmojammoja na wilaya kwa ujumla.

Na. Elisa Kapaya
Wananchi wilayani Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kuchangamkia fulsa za ufanyajibiashara katika soko la Bunazi pindi litakapokamilika ili kukuza uchumi wao na wilaya hiyo kwa ujumla.
Wito huo umetolewa Juni 20,2025 na mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali mstaafu Mayamba Maiga, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko la Bunazi katika kata ya Kassambya ambapo amesema kuwa soko hilo litachochea ukuaji wa uchumi kwa mwananchi mmojammoja na wilaya kwa ujumla.
Sauti ya kanali Mayamba Maiga mkuu wa wilaya ya Missenyi
Aidha kanali Maiga amemtaka mkandarasi atayejenga mradi huo kuumaliza kwa wakati uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa ili kuleta thamani halisi ya fedha.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi Bw.John Poul Wanga amesema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa na kampumi ya Mnico Construction (LMT) kwa miezi 18, kwa gharama ya shilingi bilioni 17.5 ambapo ujenzi wa soko hilo litajengwa kwa awamu mbili.
Sauti ya John Wanga mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni hiyo Werema Mnico, ameishukuru halmashauri ya Missenyi kwa kuiamini kampuni yake na pia ameahidi kutekeleza mradi huo kwa muda uliopangwa na kwa ubora.
Sauti ya Werema Mnico mkurugenzi wa kampuni ya Mnico Construction
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Kassambya, Christopher Kamwoma na Samia Adadi wameishukuru halmashauri hiyo kwa kuwaletea mradi huo ambao utawainua kiuchumi kupitia shughuli za kibiashara zitakazofanyika katika soko hilo.
Sauti wananchi wa kata ya Kassambya
