Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
June 21, 2025, 5:12 pm

Waendesha pikipiki (maarufu bodaboda) wilayani Biharamulo mkoani Kagera wamesisitizwa juu ya kufuata sharia za usalama barabarani ikiwemo uvaaji wa kofia ngumu ili kulinda usalama wao na abilia na kuepukana na faini wawapo barabarani.
Na.Anold Deogratias
Waendesha pikipiki (maarufu bodaboda) wilayani Biharamulo mkoani Kagera wametakiwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuhirika pamoja na kuepuka faini.
Wito huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Biharamulo, Bw.Enock Chengula, wakati akizungumza kwenye kikao cha waendesha pikipiki (maarufu bodaboda) kilichoitishwa na mabalozi wa usalama wa barabarani mkoa wa Kagera, kilichofanyika wilayani Biharamulo.

Bw. Chengula amewataka waendesha pikipiki hao kufuata sheria za uasalama barabarani ikiwemo uvaaji wa kofia ngumu (helmet) ili kujikinga na ajali lakini pia amewasisitiza juu ya kuwa na utambulisho wa maeneo wanapofanyia kazi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Kagera (RSA) Mohamed Ramadhan Makonda amewataka waendesha pikipiki hao kuvaa nguo zinazoonyesha utambulisho wao pamoja na zenye rangi maalum ili kuwasaidia kuonekana vizuri hasa nyakati za usiku.
Nao baadhi ya waendesha pikipiki wilayani Biharamulo Adinan Majdi na Allen Agustin wamesema kuwa kuna umuhimu wa uvaaji wa kofia ngumu (helmet) kwao na kwa abilia ili kulinda usalama wao.
