Kagera Community Radio

Wananchi Kyerwa watakiwa kuacha uchafuzi wa mazingira

June 10, 2025, 3:10 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa bi Zaituni Msofe

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera amewataka wakazi wilayani humo kudumisha usafi ikiwemo kuacha kutupa taka hovyo ili kuepusha magonjwa.

Na. Elisa kapaya

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Bi.Zaitun Msofe amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wilayani humo kutupa taka hovyo na kuchoma moto mbunga kwa dhana ya kupima umri wao, hali inayosababisha uharibifu wa mazingira na viumbe hai.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa, katika sherehe ya siku ya mazingira duniani ambayo ki mkoa imefanyika wilayani humo, mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa suala la uchomaji  moto mbuga limekuwa sugu hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kyerwa

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kyerwa waliohudhuria sherehe hiyo akiwemo Ester Simon,Lukasi Elias na Devota Richard wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kutunza mazingira kwa manufaa yako na kuwataka wakazi wengine kuweka mazingira yao ili kuepusha magonjwa mbali mbali pamoja na kuua viumbe hai.

Sauti za wakazi wa Kyerwa kuhusu usafi.

Naye Afisa mazingira wa wilaya ya Kyerwa Mekritrida Nchimbi amesema zaidi ya miti milioni 1 na laki saba imepandwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wilayani humo.