Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
April 23, 2025, 10:27 am

BUKOBA
Wananchi mkoani Kagera wametakiwa kutumia fursa ya madini mbali mbali yanayopatikana ktika maeneo ya kujiingizia kipato na kujikwamua na umasikini.
Hayo yameelezwa na mtaalamu wa Jiorojia Bwana Rwegoshora George wakati akizungumza na kcr fm juu ya ni kwa namna gani wananchi wa kagera wanaweza kunufaika na rasilimali walizonazo ili kujiingizia kipato.
Bwana George amesema mkoani Kagera kuna madini mengi ikiwemo mchanga wa silka ambao unatumika katika kutengeneza vioo vya magari, na madini ya kutengeneza vigae na kueleza kuwa kuna matumizi mbali mbali nje na kutengeneza voo.