Butiama FM Radio

Jamii Butiama yaonywa ukatili wa kijinsia

12 Aprili 2026, 11:50 mu

Charton Lambati kutoka Dawati la jinsia wilaya ya Butiama akizungumza na Butiama fm kupitia kipindi maalamu kuhusu ukatili wa kijinsia kinachoruka kila siku ya jumamosi asubuhi. picha na Oscar Mwakipesile

”Ukatili wa kiuchumi ni kuwa kama mimi nimeoa mwanamke ambae ni mfanyakazi lakini nikamzuia kufanya kazi kwaajili ya kulea watoto nyumbani na nikasema mimi Baba ntahudumia kila kitu maana ake nimemkatili mke wangu kiuchumi’‘Charton Lambati kutoka Dawati la jinsia wilaya ya Butiama

Na Amos Marwa

Jamii wilaya ya Butiama imeonywa kuhusu uwepo wa wimbi la ukatili wa kijinsia ikiwemo ukatili kwa watoto, ukatili wa kiuchumi na ukatili wa kingono ili kuleta usawa wa kijinsia na kupunguza madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia ikiwemo msongo wa mawazo na kuongezeka kwa watoto wa mitaani

Hayo yamebainishwa na afisa kutoka dawati la jinsia wilaya ya Butiama Charton Lambati wakati akizungumza na Butiama fm kuptia kipindi maalumu kuhusu ukatili wa kijamii na kuitaka jamii kwa ujumla kutengeneza usawa kulinda watoto na kuacha ukatili wa kijinsia.