Bunda FM Radio

Walimu pokeeni wanafunzi bila masharti yoyote

January 13, 2026, 7:30 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge akizungumza na wandishi wa habari na kutoa agizo kwa walimu wakuu wa shule za misingi na sekondari kuwapokea wanafunzi bila masharti yoyote. picha na Liwina Mnamba

Hata kama mwanafunzi hajakamilisha mahitaji yake ya shule kama vile sare za shule apokelewe asajiliwe na aendelee na masomo mwalimu mkuu atake mzuia mwanafunzi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupokonywa ukuu wa shule” Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge 

Na Amos Marwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge  amewataka  walimu wakuu wa shule za misingi na sekondari kuwapokea wanafunzi bila masharti yoyote hatakama hawajakamilisha mahitaji  yote ya shule.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaminyoge amesema kuwa walimu wanao wajibu wa kuwapokea wanafuzi wote kuanza darasa wali, la kwanza na kidato cha kwanza hatakama hawajakamilisha mahitaji ya shule ikiwemo sare za shule na kuongeza kuwa mwalimu mkuu atakae shindwa kufuata maagizo hayo atachukuliwa hatua za kisheria

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge akizungumza na wandishi wa habari na kutoa agizo kwa walimu wakuu wa shule za misingi na sekandari kuwapokea wanafunzi bila masharti yoyote.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wote watoto yenye shule ili kuanza muhula mpya wa masomo ulionza leo januari 13, 2026.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge akizungumza na wandishi wa habari na kutoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwa wakati

Aidha, amewataka wenyeviti  wa mitaa na vitongoji  kuhakikisha kwenye maeneo yao wanafunzi wanaopaswa kwenda shule wanaenda kwa wakati .

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge akizungumza na wandishi wa habari na kutoa wito kwa wenye viti wa mitaa na vitongoji kuhakikisha wanafunzi katika maeneo wanaenda shule kwa wakati

Muhula mpya wa masomo umeanza leo januari 13, 2026 na ikiwa malengo ya serikali ni kuwa ifikapo januari 30, 2026 wanafunzi wote wameripoti shuleni kwa ajili ya kwendelea na masomo yao.

Shule ya Mara girls moja ya shule za sekondari zinazopatikana wilaya ya Bunda ambapo pia wanafunzi wa kidato cha kwanza wameanza kuripoti kwa ajili ya kuanza muhula mpya wa masomo. Picha na Liwina Mnamba