Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
January 11, 2026, 7:52 pm

“Nadhani uongozi wa juu ndani ya vyama vya kisiasa ulichongia hasira Kwa vijana sisi tunajuana tunapomchagua mtu flani majina yakienda katika ngazi ya juu na huyo mtu jina lake kukatwa maanaake wanatuletea mtu wanao mtaka wao na sio maoni ya wananchi” Mseveni Sayi Chenge Mwenyekiti wa Wajasiamali kata ya Sazira
Na Amos Marwa
Wananchi na wadau mbali mbali Wilaya ya Bunda wametoa maoni yao Kwa wajumbe wa tume ya uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa amani yaliyotokea baada ya uchaguzi Oktoba 30 wilayani Bunda na kusema kuwa uteuzi wa wagombea vyama vya kisiasa kuheshimu maoni ya wananchi, vyombo vya Dola kutenda haki Kwa wananchi na malezi Bora Kwa vijana ili kuwa raia wema wanaopenda nchi yao ili wasiweze kushawishiwa kutumika vibaya na watu wasio litakia mema Taifa.
Wadau hao wameyasema hayo januari 10, 2026 kwenye mkutano wa tume hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha uwalimu Bunda uliyowahusisha wadau mbali mbali ikiwemo waathirika wa matukio hayo.

Mmoja wa wananchi akitoa maoni kwa wa jumbe wa tume ya uchunguzi wa matukio ya vurugu za Oktoba 29 siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi , Balozi Radhia Msuya na Balozi David Kapya. Picha na Amos Marwa
Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Bunda Warioba Juma Warioba aliewakilisha kundi la watoto amesema matukio ya Uvunjifu wa amani wa Oktoba 30 yalisababisha athari kubwa Kwa watoto ikiwemo msongo wa mawazo
Wajumbe wa tume hiyo, Balozi Radhia Msuya na Balozi David Kapya Waliofika kuwasikiliza wananchi Mkoa wa Mara wamewashukuru wananchi Kwa kutoa maoni na kuwaahidi kuyafanyia kazi ili kubaini chanzo Cha vurugu hizo.
