Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
January 7, 2026, 7:44 pm

”Kuna sababu nyingi za upotevu wa maji ikiwemo miundombinu kuwa chakavu, uchepushaji wa maji mita zinazotumika kwa sasa na matumizi yasiyozingatia mahitaji halisi” Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Andrea Mathew
Na Amos Marwa
Serikali imejipanga kupunguza tatizo la upotevu wa maji kwa kuweka miundombinu imara inayoendanda na nguvu ya maji ikiwemo kutoa bomba za plastiki na kuweka bomba za chuma ili kuwahakikishia wananchi huduma hiyo muda wote.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Andrea Mathew aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Mtandao wa Bomba Kutoka Migungani hadi Kaswaka iliyofanyika eneo la Mtaa wa Migungani mjini Bunda.
Kundo amewataka wananchi kuwa wazalendo na kulinda miundombinu ya maji na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wanapobaini mtu yeyote anaehusika na uharibifu huo.

Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Esther Gilyoma amesema Mamlaka inapoteza zaidi ya milioni 600 kama mapato ya upotevu wa maji kwa mwaka.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Ester Amos Bulaya amemshukuru Naibu waziri wa maji kwa kukagua miradi ya maji jimbo la Bunda mji na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza upotevu wa maji na kumtua ndoo mama kichwani.
