Bunda FM Radio

Wananchi Bunda wahakikishiwa usalama Disemba 9

December 8, 2025, 5:33 pm

Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Aswege Enock Kaminyoge, akizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali juu ya mstakabili wa amani na usalama. picha na Lewina Mnamba

Rais wa jamuhuri wa ya muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu hassan baada ya kuapishwa alisema wananchi waendelee na shughuli zao na mpaka leo hajatengua hilo hivyo nawataka wananchi kwendelea na kazi zao kama kawaida Disemba 9”. Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Aswege Enock Kaminyoge

Na Amos Marwa

Mkuu wa Wilaya ya Bunda na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Aswege Enock Kaminyoge, amewahakikishia wananchi usalama na kuwataka kwendelea na shughuli zao za kila siku kesho disemba 9

Kaminyoge ameyasema hayo baada ya mazungumzo na viongozi wa makundi mbalimbali ya ikiwemo makundi ya wajasiliamali vyama vya kisiasa na maafisa usafirishaji maarufu kama BODABODA wilya ya Bunda na kusema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuwalinda wananchi na mali zao hivyo waendelee na majukumu yao.

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge akiwataka wananchi kwendelea na shughuli zao Disemba 9

Kwa upande wao makundi mbalimbali ambayo yamewakilishwa na viongozi wao ikiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, wajasiliamali na maafisa usafirishaji maarufu kama BODABODA wamelaani maandamano hayo yanayopangwa kufanyika bila kufuata utaratibu na kusema kuwa kama wanahoja ya msingi watumie njia ya mazungumzo.

Sauti za viongozi wa makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, wajasiliamali na maafisa usafirishaji maarufu kama BODABODA.
Viongozi wa makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, wajasiliamali na maafisa usafirishaji maarufu kama BODABODA. Picha na Amos Marwa

Kwa upande wao wananchi wilaya ya Bunda wamesema maandamano hayo yasiyofuata sheria hayakubaliki kwani yanaweza kuleta machafuko na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kusima na uchumi kuyumba.

Sauti za wananchi wilaya ya Bunda wakitoa maoni yao juu ya maandamano yanayoratibiwa kufanyika disemba 9 bila kufuata sheria.

Wananchi wameendelea na shughuli zao za kila siku katika maeneo mbalimbali bila kushuhudiwa vurugu yoyote huku ulinzi na usalama ukiendelea kuimarishwa katika maeneo mbalimbali.