Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
December 6, 2025, 9:47 am

”Wazazi wapaswa kuzingatia makundi yote ya ya vyakula wakati wa kumwandalia mtoto unga lishe unakuta mzazi ameandaa mahindi, mchele, ulezi, na ngano bila kujua kuwa hicho alichokiandaa ni kundi moja la chakula ambalo ni wanga” Afisa lishe Halmashauri ya mji wa Bunda Martin Elias
Na Amos Marwa
Jamii imeaswa kuzingatia lishe, matone ya vitaminiA na dawa za Minyoo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ambazo zitafanya kinga ya watoto kuwa juu ili kupunguza changamoto ya utapia mlo mkali na udumavu wa akili.
Hayo yamebainishwa na Afisa lishe Halmashauri ya mji wa Bunda Martin Elias wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari ikiwa ni mwezi wa Afya na lishe kuanzia Disemba mosi mpaka Disemba 31 yenye kauli mbiu isemayo ”huduma bora ya afya tuwafikie watoto wote.” Martin ameongeza kuwa wazazi waache imani potofu zinazo potosha jamii juu ya huduma hizo na kuwaasa kufika vituo vya kutolea huduma za afya ili watoto wao wapate matone ya Vitani A , dawa za kutibu minyoo ya tumbo, upimaji wa hali ya lishe kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa afya ya Mtoto.