Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
December 4, 2025, 10:12 am

”Wananchi wamepunguza imani kwa serikali hivyo madiwani wenzangu twendeni tukachape kazi ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao iliyopo madarakani” Diwani wa kata ya Mcharo na mwenyekiti wa baraza la madiwani Bunda mji Masalo Minza Shani
Na Amos Marwa
Diwani wa kata ya Mcharo Masalo Minza Shani amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la madiwani halmashauri ya Mji wa Bunda.
Akisoma matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa kikao Cha kwanza Cha Baraza la madiwani katibu tawala wa Wilaya ya Bunda Salmu Alfan Mtelela kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi mkurugenzi wa Bunda Mji amesema Minza hakuwa na mpinzani hivyo wapiga kura wamepiga kura za ndio au Hapana ambapo Minza amepata kura zote za ndio 18 ambazo ni sawa na idadi ya wapiga kura.

Katibu tawala wilaya ya Bunda Salmu Alfan Mtelela alie kuwa mwenyekiti wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani akisoma matokeo ya uchaguzi picha na Amos Marwa
Akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano huo Minza ameahindi kuendeleza umoja na mshikamano ya Baraza la madiwani na kuongeza kuwa lengo lake kubwa ni kusimamia utekerezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi( CCM).
Mkutano huo wa kwanza wa madiwani pia umewapa nafasi madiwani wote kula kiapo ikiwa ni sehemu ya kuanza Rasmi majuku yao na kusema kuwa wako tayari kuwatumikia wananchi wa Mji wa Bunda kwa nafasi ya udiwani.

Mkutano huo mbali na kumchagua Mwenyekiti pia umemchagua Makamu Mwenyekiti Lucas Daniel Michael na kuchagua kamati mbalimbali zikiwemo kamati ya huduma za jamii, kamati ya mipango miji, kamati ya maadili, kamati ya kisheria na kamati ya kudhibiti ukimwi.

Baadhi ya wageni waliohudhuria katika ukumbi wa ofisi ya mkurugenzi halmashauri ya Bunda mji kwa ajili ya kushuhudia uapisho wa madiwani. picha na Lewina Mnamba